Dhamira imemsuta Karl Smith na kuamua kuvunja ukimya mahakamani akikiri kuwa ndiye aliyetekeleza mauaji yaliyosababisha pacha wake wa kufanana, Kevin Dugar kuhukumiwa kifungo cha miaka 99 jela tangu mwaka 2003 kutokana na kufananishwa.

Kwa mujibu wa Washington Post, Karl na Kevin ni mapacha wanaofana sana lakini wanatumia majina tofauti ya pili baada ya Kevin kuamua kutumia jina la ukoo la mama yake.

Alhamisi iliyopita, Karl alisimama mbele ya Mahakama ya Makosa ya Jinai ya Leighton iliyopo Chicago nchini Marekani na kutoa ushahidi huo huku machozi yakimbubujika ndugu yake.

Kevin alihukumiwa na mahakama kifungo cha miaka 99 jela kwa kosa la ujambazi wa kutumia silaha ambapo mtoto wa kiume wa miaka 6 aliuawa kwa kupigwa risasi. Tukio hilo lilitokea mwaka 2008.

Karl ambaye awali anadaiwa kumuandikia barua ndugu yake kabla ya kuingia mahakamani hapo na kumueleza ukweli kuwa yeye ndiye mhusika wa tukio hilo, alielezea kuwa tangu wakiwa watoto walikuwa wanafanya mambo mengi huku kila mmoja akivaa uhusika wa mwenzie kutokana na kufanana kwao ili watu wajue ni mtu mmoja.

“Tulikuwa tunafanya mambo na kuigiza kama mtu mmoja,” alisema Karl. “Kila nilipokuwepo alikuwepo pia, tulijifanya kama mtu mmoja. Alijifanya kuwa mimi, na nilijifanya kuwa yeye,” aliongeza.

Polisi walieleza kuwa mapacha hao walikua pamoja na walikuwa kwenye kundi la kihalifu lililojihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya.

Mama yao mzazi, ameeleza kuwa anaamini Karl hawezi kusema uongo kiasi hicho hivyo ni kweli yeye ndiye mhusika.

Kama jaji ataamua kuwa anachokisema Karl ni ukweli, kaka yake ataondolewa kifungo hicho lakini bado atakabiliwa na kesi mpya ya mauaji ya mtoto wa miaka 13 yaliyotokea Kusini mwa Chicago. Karl huenda ndiye akabeba mzigo wa kesi iliyomfunga kaka yake, hivyo wote watakuwa na hatari ya kuwa gerezani.

Aunty Ezekiel ajibu mashumbulizi ya mashabiki wake wanaosema anajipendekeza kwa Zari
Majaliwa awasimamisha kazi Maofisa Misitu wanne, Asimamisha uvunaji magogo Rufiji