Miamba ya Soka barani Afrika, Club ya Al Ahly imetangazwa rasmi kuwa bingwa wa ligi kuu nchini Misri ,huku bado wakiwa na michezo sita mkononi kabla ya ligi hiyo kumalizika.

Al Ahly wanaongoza ligi wakiwa na pointi 75 baada ya kucheza michezo 28 ,wakifuatiwa na Ismaily yenye pointi 53, Zamalek wapo nafasi ya tatu wakiwa na pointi 51,huku wapinzani wa Simba kwenye kombe la shirikisho Al Masry wapo nafasi ya 4 na pointi zao 49.

Aidha, kutokana na msimamo wa ligi hiyo hakuna timu itakayo fikisha pointi walizo nazo Al Ahly hata ikitokea wakashindwa michezo yao yote iliyo salia.

Hata hivyo, Timu hiyo imeweka rekodi mpya baada ya kufanikiwa kuchukua ubingwa wa nchi hiyo kwa mara ya 40.

Wananchi wenye hasira kali wachoma moto gari
Moise Katumbi atangaza kugombea Urais

Comments

comments