Kikosi cha Al Ahly kimewasili jijini Dar es salaam, mapema hii leo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNIA) tayari kwa mchezo wa mkondo wa kwanza wa ligi ya mabingwa barani Afrika.

Mafarao hao waliamua kutua kama mabubu na kuwa wagumu kuongoea chochote na wanahabari wachache waliokuwepo uwanjani hapo.

Hata hivyo haikufahamika kwa nini waliamua kuwasili nchini kwa style hiyo, jambo ambalo liliwaacha katika hali ya mshangao mkubwa baadhi ya waandishi waliokuwepo uwanjani hapo.

Waarabu hao wamewasili na kikosi cha zaidi ya watu 50 wakiwemo wachezaji, madaktari, maafisa wa FA ya Misri pamoja na waandishi wa habari.

Al Ahly 04

Miongozi wa wachezaji hao ni pamoja na wale saba wanaoitumikia timu ya taifa ya Misri wakiwemo viungo Karim Bambo, Ramadan Sobhy, Saleh Gomaa, washambuliaji ni Omar Bassam, walinzi ni Ramy Rabia na Ibrahim Hassan pamoja na mlinda mlango Mossad Awad, wakiongozwa na kocha kutoka nchini Uholanzi Martin Jol.

Al Ahly 02

Mchezo wa mkondo wa kwanza kati ya Al Ahly dhidi ya mabingwa wa soka Tanzania bara, Young Africans utachezwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam siku ya jumamosi.

Young Africans ambao wameweka kambi kisiwani Pemba kwa ajili ya mchezo huo, watatakiwa kushinda mchezo huo wa mkondo wa kwanza ili kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kupambana watakapokwenda jijini Cairo majuma mawili yajayo.

Dk. Shein amtosa Rasmi Maalim Seif
Rais Mpya wa FIFA akumbwa na Kashfa ya Rushwa, ashinikizwa kujitumbua Jipu