Wachezaji wa klabu ya  Al Masry ya Misri jana walishindwa kumaliza mchezo wa mkondo wa pili wa nusu fainali wa michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya AS Vita ya DR Congo, kwa kisingizio cha kutopendezwa na maamuzi ya mwamuzi wa mchezo huo, Bernard Camille kutoka visiwa vya Shelisheli.

Tayari Al Masry walikua wameshafungwa mabao manne kwa sifuri, kabla ya kufanya maamuzi ya kuondoka sehemu ya kuchezea ya uwanja wa ugenini.

Wachezaji wa Al Masry walichukua maamuzi ya kuondoka katika sehemu ya kuchezea dakika ya 75, baada ya kocha wao Hossam Hassan kumlalamikia mwamuzi, kwa madai alikua hawatendei haki.

Malumbano hayo yaliyotokana na hisia za kuonewa, yalianza baada ya Jean-Marc Makusu kufunga bao la nne, ambapo Al Masry walidai halikua halali, kwa kuamini mchezaji huyo alikua ameotea kabla ya kutumbukiza mpira wavuni.

Baada ya kutoka uwanjani kwa wachezaji wa Al Masry, mwamuzi alisubiri kwa dakika tano na baadae alipuliza kipyenga cha kuashiria kumalizwa kwa pambano hilo na kuiwezesha AS Vita kupata ushidni wa mabao manne kwa sifuri.

Image result for AS Vita Club 2018Kikosi cha AS Vita Club

Kwa ushindi huo AS Vita wametinga hatua ya fainali ya michuano hiyo, na watapambana na Raja Casablanca ya Morocco mwezi ujao.

Wawakilishi hao wa Morocco wamefuzu kucheza fainali ya kombe la shirikisho barani Afrika, baada ya kuibanjua Enyimba ya Nigeria mabao mawili kwa moja katika mchezo wa mkondo wa pili uliounguruma jana Jumatano, na kabla ya hapo walifaniiwa kushinda bao moja kwa sifuri nyumbani kwao, hivyo wamesonga mbele kwa jumla ya mabao matatu kwa moja.

Kwenye mchezo wa fainali mkondo wa kwanza ambao utachezwa Novemba 25, Raja Casablanca wataanzia nyumbani kwao na juma moja baadae watakwenda kumalizia mjini Kinshasa-DR Congo mchezo wa mkondo wa pili.

Ubelgiji yaipiku Ufaransa, Cape Verde yaibeba Tanzania viwango vya ubora wa soka
Trump avishambulia vyombo vya habari, avitaka viache kupotosha