Wachezaji wanane wa kikosi cha kwanza cha Al Merrikh wanadaiwa kupatikana na maambukizi ya virusi vya Corona muda mfupi kuelekea pambano dhidi ya Simba SC.

Mchezo huo utachezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, kuanzia saa kumi jioni.

Wachezaji hao wanaodaiwa kukutwa na maambukizi ni Abdul Rahman Karango, Al Taj Yaqoub, Bakhit Khamis, Ramadan Ajab, Tony, Bakri Al Madina, Saif Al Damazin na Imad Abdel Moneim.

Hata hivyo kwa mujibu wa vyombo mbalimbali vya Habari nchini Sudan, Al Merrikh imeandika malalamiko ya dharura kwa Shirikisho la Soka Barani Afrika kuituhumu Simba SC kughushi matokeo ya vipimo.

Taratibu wa upimaji wa virusi vya Corona zinaendeshwa chini ya Shirikisho la soka Barani Afrika ‘CAF’, hivyo malalamiko ya Al Merrikh huenda yakawa na walakini.

Metacha: Nitawachukulia hatua za kisheria
Velud aikana Young Africans