Wizara ya sheria nchini Libya imethibitisha kuachiwa kwa Al-Saad Gaddafi mtoto wa aliyekuwa Rais wa zamani wa Libya Moammar Gaddafi, kutoka gerezani baada ya kukaa Zaidi ya miaka saba.

Al-saadi ambaye ni mchezaji wa zamani wa mpira wa miguu nchini Italia , alikuwa ameshikiliwa katika  gereza la Tripoli kwa Zaidi ya miaka saba kutokana na kukabiliwa na tuhuma za uhalifu dhidi ya waandamanaji na mauaji ya kocha wa mpira wa miguu wa Libya Bashir Al-Rayani mwaka 2005.

Taarifa kutoka Libya zinaeleza kuwa kuachiliwa kwa  Saadi Gaddafi kumetokana na mazungumzo ambayo yalikuwa pamoja na wakuu wa kabila,Waziri Mkuu Abdul Hamid Dbeibeh na Waziri wa zamani wa mabo ya ndani Fathi Bashagha

Ripoti zinaeleza kuwa Saadi  amesafiri kwenda nchini Uturuki baada ya kuachiwa huru.

Biteko asisitiza leseni machimbo madogo ya madini
Dunia yalaani Mapinduzi Guinea