Kikundi cha wanamgambo wa Al-Shabaab kutoka nchini Somali kimekuwa tishio kubwa kwa usalama kaskazini mwa Kenya, ambapo kimesababisha walimu wengi kuomba kuhamishwa vituo vyao vya kazi kufuatia kuuawa kwa walimu watatu mwezi februari mwaka huu.

Walimu hao wamesema kuwa wamefikia hatua ya kutoroka vituo vyao vya kazi kwa madai kuwa wenzao waliuawa kwa itikadi za kidini, ambapo wamesema kuwa tatizo hilo limekuwa sugu.

Aidha, Walimu walianza kulikimbia eneo hilo mwaka 2015, kufuatia mauaji ya zaidi ya wanafunzi 140 katika chuo Kikuu cha Garissa tukio lililowafanya walimu na wafanyakazi wengine wa umma wasio Waislamu kuhisi wako hatarini.

Hata hivyo, Tangu mwezi Februari mwaka huu Tume ya Taifa ya Walimu imeidhinisha zaidi ya maombi hamsini ya kuhamishwa walimu kutoka eneo hilo, jambo lililoibua pingamizi miongoni mwa wakaazi na baadhi ya viongozi wa eneo hilo.

 

Ndugai adai Bunge haliwezi kuidhinisha fedha za matibabu ya Lissu
Siwa ya Bunge la Nigeria yapatikana baada ya kuibiwa