Kufuatia shambulio lililotokea nchini kenya jijini Nairobi la mlipuko wa mabomu na kufyatuliwa kwa risasi katika hoteli ya kifahari ya DusitD2 iliyoko mtaa wa Riverside, kundi la kigaidi la Al-shabab wamekiri kuhusika katika shambulio hilo.

Taarifa hiyo imetolewa na chombo cha habari cha BBC ikisema kuwa muda mchache mara baada ya kutokea kwa shambulio hilo kundi la kigaidi la Al-shabab liliipigia simu chombo hicho cha habari na kusema kuwa kundi hilo limehusika katika operesheni inayoendelea Nairobi.

Na Kundi hilo limedai kuwa litatoa taarifa kamili mara baada ya operesheni yao kukamilika.

Aidha shambulio hilo limesababisha baadhi ya watu kujeruhiwa vibaya na tayari vyombo vya usalama vimeshawapeleka hospitali majeruhi hao kwa ajili ya matibabu zaidi.

Baadhi ya watu waliokwama kwenye vyumba vya jumba hilo wamekuwa wakiandika ujumbe kwenye mitandao wa kijamii wakieleza kwamba wamekwama, au kujificha.

ShambulioShambulioShambulio

CCM Njombe wamng'ata sikio mwenyekiti wa chama hicho Iringa
Breaking: Magaidi wavamia hoteli Nairobi, wafyatua risasi na mabomu