Kundi la kigaidi la Al-Shaba limesema kuwa limewaua wapelelezi watatu wa Marekani pamoja na mmoja wa Uingereza.

Kwa mujibu wa tovuti ya kundi hilo, wapelelezi hao walikuwa kati ya watu watano waliouawa kikatili kwa kupigwa risasi hadharani, Jumanne wiki hii.

Kundi hilo limedai kuwa watu hao waliuawa baada ya kukiri kuwa wamekuwa wakitoa taarifa kwa Uingereza na Marekani kuhusu watu wanaoliunga mkono waishio Uingereza.

Wamedai kati ya watu hao, mmoja alibainika kuwa alikuwa anafanya kazi na Serikali ya Somali.

Imeelezwa kuwa wapelelezi hao walihusika kuweka vifaa vya kunasa sauti kwenye gari la msafara wa Al-Shabab, vilivyosaidia Marekani kushambulia msafara huo kwa kutumia ndege zisizo na marubaini.

Reuters wameripoti kuwa walifanya mazungumzo na msemaji wa kundi hilo ambaye alithibitisha kuwa taarifa hizo ni za kwao.

Hata hivyo, Serikali ya Marekani na Uingereza hazijazungumza lolote kuhusu taarifa hizo.

Marekani na Uingereza hivi karibuni zilifanya mashambulizi makali kwenye ngome za Al-Shabab, mashambulizi ambayo yameripotiwa kulidhoofisha zaidi kundi hilo.

Kundi la Al-Shabab ambalo ni sehemu ya kundi la A-Qaeda, lilifukuzwa katika mji mkuu wa Mogadishu mwaka 2011, baada ya vikosi vya Serikali ya Somali vikishirikiana na vikosi vya Umoja wa Afrika kufanya oparesheni maalum dhidi yake.

Mbunge mwingine wa Chadema ajiuzulu
Breaking: Mo Dewji atekwa na watu wasiojulikana