Meneja wa klabu ya Crystal Palace Alan Pardew yupo kwenye hatari ya kupoteza ajira yake, endapo atashindwa kuibuka na ushindi katika mchezo wa mwishoni mwa juma hili dhidi ya Swansea City.

Mwishoni mwa juma lililopita Pardew alishuhudia kikosi chake kikishindwa kufurukuta dhidi ya Man City kwa kukubalia kichapo cha mabao mawili kwa moja, matokeo ambayo yameendelea kuzaimisha klabu hiyo katika msimamo wa ligi ya nchini England, ambapo kwa sasa inashika nafasi ya 16.

Mtihani kwa babu huyo mwenye umri wa miaka 55 umetolewa na mmiliki mpya wa Crystal Palace Josh Harris, ambaye inasemekana anakerwa na mwenendo wa kikosi chake ambacho mpaka sasa kimeshapoteza michezo saba, kushinda mitatu na kutoka sare mara mbili.

Aliyekua kocha mkuu wa timu ya taifa ya England Sam Allardyce ameanza kutajwa kuchukua nafasi ya Pardew kama itatokea anashindwa kufikia lengo la kufanya vyema huko Selhurst Park.

Allardyce alitangaza kujiuzulu nafasi ya ukuu wa benchi la ufundi la timu ya taifa ya England, kufutia kashafa ya kutoa siri za waajiri wake (FA) kwa waandishi wa habari ambao walijifanya wafanyabiashara.

Mwingine anaetajwa huenda akapewa nafasi ya kumrithi Pardew ni kocha mkuu wa timu ya taifa ya Wales Chris Coleman, ambaye aliwahi kuitumikia Crystal Palace kama mchezaji kuanzaia mwaka 1991hadi 1995.

Hata hivyo mtihani mkubwa kwa Coleman kupewa ajira klabuni hapo, utakua ni kuvunja mkataba wake mpya na chama cha soka nchini Wales ambao aliusaini miezi kadhaa iliyopita.

Kocha huyo alisaini mkataba wa miaka miwili baada ya fainali za mataifa ya Ulaya (Euro 2016) ambapo alikiongoza kikosi cha Wales hadi katika hatua ya nusu fainali.

Uamuzi Wa Kamati Ya Saa 72 Ya Uendeshaji Na Usimamizi Wa Ligi
Serikali kuhifadhi kumbukumbu za urithi usioshikika