Aliyekua meneja wa klabu ya Fiorentina, Aldo Agroppi amekiri kushtushwa na ada ya usajili ambayo Man Utd wapo tayari kulipa kwa ajili ya kumnasa kiungo kutoka nchini Ufaransa na klabu ya Juventus, Paul Pogba.

Man Utd wameonyesha kuwa tayari kulipa kiasi cha Euro milioni 120, ili kufanikisha azma ya kuremjesha kiungo huyo mwenye umri wa miaka 23 huko Old Trafford ambapo aliondoka mwaka 2012, baada ya kukosa nafasi katika kikosi cha kwanza.

Agroppi ameuambia mtandao wa TMW, hakuamini pale aliposikia taarifa za ada ya usajili wa Pogba ambayo anaamini inatosha kwa viongozi wa Juventus kukubali kumuachia kiungo huyo kuondoka na kurejea Old Trafford.

Amesema ni nadra sana kwa klabu kama Man Utd kujihukumu yenyewe katika suala la usajili, hivyo hakuna haja kwa katika usajili wa kiungo huyo, kuendelea kuchukua muda mrefu na badala yake ameshauri limalizwe mapema.

Hata hivyo Agroppo ametoa angalizo kwa viongozi wa Juventus, kwa kuwaambia soka lina mambo mengi na huenda mpango huo ukayeyuka mara moja kutokana mzingira yaliopo, hivyo ni vyema wakakubalia kuafiki ofa iliyowafikia mikononi mwao.

“Inafurahisha kuona klabu inajipangia kiasi cha kumnunua mchezaji kama Pogba, na ninawashauri viongozi wa Juventus kulimaliza jambo hili na kuangalia mambo mengine katika kipindi hiki cha majira ya kiangazi!

Taarifa za Pogba kuwa mbioni kuihama Juventus, zimetawala katika vyombo vya habari dunaini kote tangu jana, baada ya uongozi wa The Old Lady kukubali kumuuza kiungo huyo kwa ada ya usajili wa Pauni milioni 100.

Tailor Swift afunika mastaa walioingiza pesa nyingi zaidi, Jackie Chain naye yumo
Carlo Ancelotti Asisitiza Kuondoka Kwa Mario Gotze