Wachazaji wanaocheza katika ligi ya nchini England Alex Iwobi na Victor Moses wametajwa kwenye kikosi cha wachezaji 30 cha timu ya taifa ya Nigeria, kitakachoingia kambini kujiandaa na fainali za kombe la dunia, zitakazoanza Urusi, Juni 14.

Wawili hao wanazitumikia klabu za jijini London (Arsenal na Chelsea) wamejumuishwa kwenye kikosi hicho na kocha Gernot Rohr, huku wakiaminiwa huenda wakawa viongozi wazuri kwa wachezaji wengine kuelekea katika fainali hizo.

Hata hivyo kocha Gernot Rohr raia wa Ujerumani, atalazimika kupunguza wachezaji watano ili kusalia na wachezaji 25, ambao kisheria wanaruhusiwa kuunda kikosi kitakachoshiriki fainali za kombe la dunia nchini Urusi.

Kabla ya kufanya maamuzi ya kupunguza kikosi hadi kufikia wachezaji 25, Nigeria itacheza michezo ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya DR. Congo, England na Jamuhuri ya Czech Republic.

Kikosi cha Nigeria kilichotajwa leo, tayari kwa mshike mshike wa fainali za kombe la dunia upande wa makipa ni: Francis Uzoho (Deportivo La Coruna, Spain); Ikechukwu Ezenwa (Enyimba FC); Daniel Akpeyi (Chippa United, South Africa), Dele Ajiboye (Plateau United)

Mabeki: Abdullahi Shehu (Bursaspor FC, Turkey); Tyronne Ebuehi (Ado Den Haag, The Netherlands); Olaoluwa Aina (Hull City, England); Elderson Echiejile (Cercle Brugge KSV, Belgium); Brian Idowu (Amkar Perm, Russia); Chidozie Awaziem (Nantes FC, France); William Ekong (Bursaspor FC, Turkey); Leon Balogun (FSV Mainz 05, Germany); Kenneth Omeruo (Kasimpasa FC, Turkey); Stephen Eze (Lokomotiv Plovdiv, Bulgaria)

Viungo: Mikel John Obi (Tianjin Teda, China); Ogenyi Onazi (Trabzonspor FC, Turkey); Wilfred Ndidi (Leicester City, England); Oghenekaro Etebo (Las Palmas, Spain); John Ogu (Hapoel Be’er Sheva, Israel); Uche Agbo (Standard Liege, Belgium); Joel Obi (Torino FC, Italy), Mikel Agu (Bursaspor FC, Turkey)

Washambuliaji: Ahmed Musa (CSKA Moscow, Russia); Kelechi Iheanacho (Leicester City, England); Moses Simon (KAA Gent, Belgium); Victor Moses (Chelsea FC, England); Odion Ighalo (Changchun Yatai, China); Alex Iwobi (Arsenal FC, England); Junior Lokosa (Kano Pillars, Nigeria); Simeon Tochukwu Nwankwo (Crotone, Italy)

Guerrero aongezewa kifungo, kukosa kombe la dunia
Jorge Sampaoli atangaza jeshi la Argentina

Comments

comments