Beki wa pembeni wa mabingwa wa soka nchini Italia Juventus Alex Sandro, amerejea kwenye rada za klabu ya Man Utd, ambayo imedhamiria kuboresha kikosi chake itakapofika mwezi Januari mwaka 2019, wakati wa dirisha dogo la usajili.

Taarifa kutoka ndani ya klabu ya Man Utd zinaeleza kuwa, pamoja na uongozi wa klabu hiyo kufanikisha mpango wa kumsainisha mkataba mpya beki wa kushoto Luke Shaw siku za hivi karibuni, bado inaaminika usajili wa Sandro endapo utafanikiwa, utaleta changamoto kubwa katika safu ya ulinzi.

Meneja Jose Mourinho amekua mstari wa mbele kuhakikisha mpango wa usajili wa beki huyo kutoka nchini Brazil, unapewa nafasi kubwa wakati wa usajili wa majira ya baridi (Mwezi Januari).

Taarifa nyingine zinadai kuwa, huenda Man Utd wakamuhusisha kiungo kutoka nchini Ufaransa Paul Pogba katika dili la kufanikisha wanampata Sandro kwa urahisi.

Mahusiano hafifu kati ya kiungo huyo, ambaye alikua sehemu ya kikosi cha Ufaransa kilichotwaa ubingwa wa dunia mwezi Julai mwaka huu, dhidi ya mkuu wa benchi la ufundi la Man Utd Jose Mourinho yanatajwa kupunguza mahusiano baina ya wawili hao, na suluhisho ni kuhakikisaha anaondoka kikosini.

Kwa upande wa Italia, taarifa zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari zinadai kuwa, Juventus nao wamejipanga kufanikisha mpango wa kumsajili kwa mara nyingine Pogba mwezi Januari mwaka 2019.

Njia mbadala inayotajwa huenda ikatumika, ni usajili wa mkopo wa miezi sita, ambao unaaminiwa huenda ukamuondoka kiungo huyo kwenye majanga ya kuishi mazingira magumu dhidi ya Mourinho.

Majaliwa atoa agizo kuhusu eneo la Kata ya Kiomoni
Askofu ataka mishahara ikatwe zaka moja kwa moja