Klabu ya Arsenal itamkosa mshambuliaji wake kutoka nchini Ufaransa, Alexandre Lacazette kwa muda wa majuma  sita kutokana na mchezaji huyo kusumbuliwa na jeraha la goti la kushoto.

Arsenal imethibitisha juu ya majeraha hayo ya Lacazette ambaye ni raia wa Ufaransa, ambapo aliumia Jumanne ya wiki hii.

Arsenal imesema tatizo alilopata siyo kubwa lakini atalazimika kuwa nje kwa muda huo wa wiki nne hadi sita ili kupona kwa uhakika.

Lacazette alikosa nafasi mbili za wazi wakati timu yake ilipofungwa bao 1-0 na Tottenham, Jumamosi iliyopita kitendo kilichowakasirisha baadhi ya mashabiki wa timu yake.

Mbali na hapo amekuwa akikabiliwa na ushindani mgumu wa namba tangu Pierre-Emerick Aubameyang alipotoa Arsenal hivi karibuni kwa ada ya pauni milioni 56 akitokea Borrusia Dortmund.

Fuvu la kichwa lamuweka pembeni Ryan Mason
Idd Cheche: Hatujakata tamaa ya ubingwa VPL

Comments

comments