Mchezaji mpya wa klabu ya Manchester United, Alexis Sanchez amehukumiwa kwenda jela miezi 16 kutokana na kosa la kukwepa kulipa kodi.

Hukumu hiyo imetolewa mara baada ya kugundulika kukwepa kulipa kodi wakati alipokuwa nchini Hispania ambapo imebainika kuwa anadaiwa kiasi cha pauni laki tisa.

Aidha, Kwa mujibu wa sheria za Hispania, hukumu ya kosa hilo haizidi miaka miwili jela au kulipa pauni 525,000 kutokana na kosa ambalo alilifanya miaka mitatu alipokuwa akichezea klabu ya Barcelona.

Hata hivyo, Hukumu hiyo imekuja katika kipindi ambacho bado mamlaka ya mapato nchini humo ikifanya uchunguzi dhidi ya kocha, Jose Mourinho anaye tajwa kufanya kosa kama hilo.

LIVE: Yanayojiri Bungeni Dodoma leo Februari 9, 2018
Video: Tambwe wa Chadema alivyokufa ghafla, Mawaziri sita wabanwa

Comments

comments