Mshambuliaji wa klabu ya Arsenal Alexis Sanchez amepatwa na majeraha ya misuli ya kiazi cha mguu, akiwa katika kati ya timu ya taifa lake la Chile, ambayo inajiandaa na michezo ya kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia.

Taarifa zilizothibitishwa na shirikisho la soka nchini Chile zimeeleza kuwa, mshambuliaji huyo atafanyiwa vipimo hii leo, ili kujua kama ataweza kuuwahi mchezo dhidi ya Colombia na kisha Uruguay.

Kitengo cha utabibu ambacho kipo chini ya shirikisho la soka nchini Chile kimepewa jukumu la kuhakikisha majibu ya vipimo vya Sanchez yanapatikana haraka iwezekanavyo.

Hata hivyo Sanchez ataendelea kubaki mjini Santiago, kwa ajili ya matibabu ya awali, na kama mambo yataendelea kuwa tofauti na kufikia hatua ya kushindwa kujumuika na wenzake kwenye michezo hiyo miwili, atalazimika kurejeshwa jijini London katika klabu yake ya Arsenal.

Taarifa za kuumia kwa Sanchez, huenda zikawa pigo kwa meneja Arsene Wenger ambaye kwa sasa anaupigia hesabu mchezo ujao wa ligi kuu ya soka nchini England ambapo The Gunners watasafiri kuelekea mjini Manchester, kwa ajili ya kupambana na Man Utd, Novemba 19.

Toni Kroos Kuzikosa Atletico Madrid, FC Barcelona
Cristiano Ronaldo Atwaa Tuzo Hispania