Meneja wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger, ametoa tahadhari kwa viongozi wa benchi la ufundi la timu ya taifa ya Chile kuhusu afya ya mshambuliaji Alexis Sanchez ambaye anakabiliwa na majeraha ya kiazi cha mguu.

Wenger amesema benchi la ufundi la timu ya taifa ya Chile linapaswa kuwa makini na mshambuliaji huyo, ili kuondoa mashaka ya kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu.

Wenger amesema kuna haja kwa kocha mkuu wa Chille Juan Antonio Pizzi kuwa makini, na hatopendezwa kuona akimtumia katika mchezo ujao wa kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia dhidi ya Uruguay siku ya jumanne.

“Nilipata ujumbe kutoka kwa kocha Pizzi akiniarifu kuhusu kuumia kwa Sanchez,” Alisema Wenger alipozungumza na beIN Sports.

“Tunatarajia kujiridhisha sisi wenyewe kwa vifaa vyetu hapa (Arsenal) kwa kumfanyia vipimo Sanchez na haturidhishwi na maelezo yaliyotolewa na Pizzi kuhusu matarajio ya mchezaji huyo kuwa katika nafasi nzuri ya kucheza juma lijalo.

“Itakua ni muhimu kwa Arsenal kujua tatizo lilikua ni nini hadi kuumia kwa Sanchez, ili tufahamu pakuanzia kuhusu matibabu yake, na nisingependa kuona analazimishwa kucheza kwa sababu za kuwafurahisha watu wachache.”

Msimu uliopita Sanchez alikosa karibu miezi miwili kucheza soka, kufuatia kuumia misuli ya paja, jambo ambalo Wenger anaamini lilichangia kuyumba kwa kikosi chake na kushindwa kufikia lengo la kutwaa ubingwa wa England.

Diego Costa Kuikosa England
Stefano Pioli Kumsajili Matteo Darmian