Mfalme Kiba, ameamsha shangwe kwa mashabiki wake baada ya kutangaza ujio wake mpya akiwa na chuma alichokiita ‘Hela’.

Kupitia Instagram, Ali Kiba ameweka picha inayotangaza ujio wa ngoma hiyo, picha ambayo inamuonesha mtu aliyejifunika sura kwa bandana na kuvalia mawani yaliyompa ‘uso wa kazi.’

Ngoma hii itakuwa karata ya Kiba inayofuatia ‘Mvumo wa Radi’ uliovuma na mengi ikiwa ni pamoja na ndoa, kinywaji cha Mo Faya na sakata la kudukuliwa kwa video yake YouTube.

Kiba ambaye hivi sasa ni mchezaji rasmi wa Costal Union, aliomba nafasi ya kupumzishwa katika michezo kadhaa ili aweze kufanya mazoezi zaidi kabla ya kuingia tena uwanjani.  Lakini mapumziko hayo kwenye soka yanampa nafasi ya kutimua vumbi lingine kwenye muziki.

Kiu ya mashabiki wa Kiba sasa iko kwenye kiwango cha juu, kiasi ambacho wameifuata post yake ya pili anayoupa shavu wimbo mpya wa Ray C na kuendelea kukazia kuhusu mtoko wa ‘Hela’.

 

View this post on Instagram

 

#KingKiba

A post shared by alikiba (@officialalikiba) on


Je, Hela itakuwa chuma cha aina gani katikati ya vyuma ambavyo wasanii kadhaa wameachia katika kipindi hiki?

Tunasubiri kama wewe unavyosubiri, lakini tutakuwa wa kwanza kukujuza yaliyomo. Endelea kuwa hapa.

Walimu 7 wafutwa kazi, wengine walimwa barua
Navy Kenzo wajiunga WCB baada ya 'Katika' na Diamond?