Ali Kiba anaendelea kuzivuta collabo za wasanii wakubwa duniani, ambapo sasa amepanga kufanya kitu kingine kikubwa na Mfalme wa R & B duniani, R. Kelly.

R kelly

Kiba na R- Kelly walikutana kwa mara ya kwanza kwenye mradi wa One 8 uliowashirikisha wasanii wengi wakubwa wa Afrika ampapo walirekodi wimbo wa ‘Hands Across the World’. R Kelly alimtaja Msanii huyo wa Tanzania kama ‘the best vocalist’ wa mradi huo.

Mkali huyo wa ‘Mwana’ leo ameiambia The Playlist ya 100.5 Times Fm kuwa amewasiliana na R-Kelly hivi karubuni na wamepanga kufanya kitu kikubwa pamoja.

“Nimewasiliana na R. Kelly hivi karibuni… tumepanga kufanya kitu fulani, siwezi kusema sasa hivi ni kitu gani lakini tujiandae tu muda ukifika watakipata,” Ali Kiba aiiambia The Playlist ya Times Fm.

Hivi karibuni, Ali Kiba aliingia studio na kufanya wimbo na Ne-Yo aliyekuwa jijini Nairobi nchini Kenya kwa ajili ya mradi wa Coke Studio.

Ali Kiba na Neyo

 

Haya ni Mambo ambayo hupaswi ‘kuya-google’
Vurugu zavunja uchaguzi wa Meya wa jiji la Dar, Polisi wawazima Ukawa