Ali Kiba ameweza kugusa kiwango cha wasanii wakubwa duniani baada ya kufanikiwa kufanya kazi na mwalimu wa kucheza (Choreographer), Oththan Burnside aliyefanya kazi zilizotukuka na wasanii hao wakubwa.

Burside alikuwa wa kwanza kutoa taarifa hiyo njema kwa mashabiki wa muziki duniani kupitia akaunti yake ya Instagram.

Burnside (Kushoto), Ali Kiba (Kulia)

Burnside (Kushoto), Ali Kiba (Kulia)

“Excited to be working with @officialalikiba #EastAfrica #KingKiba your in great hands! OtheezyCreatedIt #CreativeDirector #Choreographer S/O @msaagency @Brandonlouisla!!! #MSASquad #MSAFAM thank you guys,” Burnside aliandika.

Ali Kiba alijibu post hiyo, “Excited to be working with you too . See you in a bit.”

Kazi alizowahi kufanya Burnside kwa kuongoza mtindo wa kudance kwenye  ziara za muziki za wasanii wakubwa ni pamoja na Rihanna (Diamond World Tour) Ciara (Jackie Tour), Miley Cyrus (Bangerz World Tour), Keyshia Cole (Point of No Return), Usher (OMG Tour) Britney Spears (Til The World Ends World Tour) Ne-Yo (Scream Tour) na zingine.

Nyingine ni video za muziki kama Believer ya Keyshia Cole, Champion ya Mila J, Come With Me ya Ne-Yo, Loyal ya Chris Brown,    I Got It ya Ashanti ft. Rick Ross, Turn It Up ya Sean Paul, Love More ya Chris Brown ft. Nicki Minaj, Pour It Up ya Rihanna, Boyfriend ya Justin Bieber, Automatic ya Dawn Richard.

Burnside alishiriki katika uchezaji wa kwenye filamu kadhaa zikiwemo Stomp The Yard na School Dance.

Bila shaka kazi zinazokuja za Ali Kiba zitakuwa na viwango vya hali ya juu katika uchezaji kwa kuwa amelipata jembe linalolima na kuaminika duniani kwa kuvunja.

Dkt. Magufuli Aapishwa Rasmi Kuwa Rais wa Tanzania, JK astaafu Rasmi
Walichoamua Ukawa Kuhusu Kuapishwa Dkt. Magufuli