Uhasimu kati ya Ali Kiba na Diamond umechomoza tena hadharani baada ya mkali huyo wa ‘Aje’ kuitupia lawama timu ya hasimu wake huyo kwa kukatishwa kwa show yake jijini Mombasa alipokuwa akimsindikiza Chris Brown.

Ali Kiba ambaye alijikuta akishindwa kuendelea na show jukwaani na kulazimika kuondoka baada ya kikuza sauti (microphone) yake kukatwa sauti, amedai kuwa anahisi alifanyiwa hujuma kwani alimuona meneja wa Diamond nyuma ya jukwaa hilo wakati yeye akiendelea kuimba, kitu ambacho anadai sio cha kawaida.

“Nilimuona meneja wake Diamond alikuwepo pale, anafuata nini backstage wakati mimi naperform, yeye anahusika kama nani? Haileti picha nzuri,” Ali Kiba aliiambia Mseto East Africa.

“Kwasababu hata kama watu wanafikiria kwamba of course hatuna beef lakini sasa umefuata nini na vitu kama hivyo vina-happen, wewe unafikiria watu watafikiria nini? Kitu gani kimemfanya aje? Kuna watu wengi waliokaa kwenye VIP unaweza ukaangalia show, kuja kwenye show, kaa kwenye VIP, angalia show. But alikuwa anafanya nini backstage wakati mimi naperform?” alihoji.

Alisema kuwa ingawa kiu ya mashabiki kwa show yake ilikuwa kubwa sana na muda mwingi walikuwa wanamuita apande jukwaani, alishangaa kuona anakatiwa microphone.

Hata hivyo, Ali ambaye aliitwa tena jukwaani kuimba bila ‘live band’ baada ya kumalizika kwa show ya Chris Brown, anahisi kuwa huenda pia ratiba ya Chris Brown kutakiwa kupanda jukwaani haraka ili aondoke ndani ya muda wa makubaliano ulipelekea yeye kukatiwa mic.

Bado upande wa Diamond haujatoa neno rasmi kuhusu tuhuma hizo lakini mashabiki wa timu hizo mbili wameendelea kuwashiana moto kwenye mitandao ya kijamii.

Samsung wawataka wateja wao kutupa ‘Galaxy Note 7’, zina tatizo la kulipuka kwenye chaji
Gari la kwanza kutengenezwa na kampuni ya Kitanzania kuzinduliwa Desemba 2016