Ni kama Mfalme ameghafilishwa na yanayosemwa kwenye mitandao ya kijamii na ameamua kuliamsha dude kwa hasira alizonazo.

Leo, mitandao ya kijamii na vijiwe vya burudani vimeubeba mjadala mzito wa mashairi yaliyo kwenye Fresh Remix iliyonogeshwa na rap ya Bosi wa WCB, Diamond Platinumz aka Simba ambaye amesikika akiunguruma kama Simba anayetamba kwenye himaya ya mbuga yake.

Baada ya kutweet akieleza kuwa anajua anachukiwa, japo hakumtaja jina, sasa Ali Kiba ameonesha kujibu moja kwa moja mashairi ya Diamond kwenye Fresh Remix, yaliyosikika, “Viuno vidogo wanataka pensi ya Pepe Kale, Si walitaka Kiti… nimewapa hadi kitanda wakalale.”

““The KING ll always Be a KING. je Umeshakitandika nilale MALKIA wangu wa nguvu ?? #KingKiba,” Kiba ametweet.

Ingawa hakumtaja jina, tweet hii inadalili zote kuwa inalenga kujibu alichokisema Diamond, “Mlitaka kiti, nimewapa hadi kitanda mkalale.”

Diamond anahusishwa na ‘kutaka kiti’ kufuatia kauli yake kuwa anarejea na kiti chake hakijakaliwa na mtu, hivyo Mfalme anakifuta vumbi tu.

Justine Bieber avunja urafiki na Mayweather kisa ‘Upako’
Galatasaray Kubisha Hodi Kaskazini Mwa London