Mkali wa Aje, Mfalme Kiba amejibu kauli ya hasimu wake, Diamond Platinumz aliyoielekeza kwake kuhusu uvaaji wa pete ya kijani.

Wiki iliyopita, akifanya mahojiano na XXL ya Clouds Fm, Diamond alirusha makombora mengi dhidi ya Ali Kiba na Ommy Dimpoz huku akitaja uvaaji wa pete ya kijani kama moja kati ya sababu inayomtofautisha na washindani wake.

“Mimi sina matatizo na watu ndio maana wakijaribu kushindana na mimi huwa wanashindwa. Hata ukiniangalia sina hata pete ya kijani kwenye vidole vyangu,” Diamond alifunguka

Leo, Ali Kiba amepost picha ya kejeli kwenye Instagram na kuandika maelezo yanayoicheka kauli hiyo ya Diamond.

“officialalikibaPete Ya Kijani ?? @Fadiboi5d #BirthdayLoading29thNoV #KingKiba” aliandika.

Pete Ya Kijani ?? ? @Fadiboi5d #BirthdayLoading29thNoV #KingKiba

A photo posted by alikiba (@officialalikiba) on


 

Uhasama kati ya Ali kiba na Diamond uliwekwa wazi rasmi wiki hii kupitia XXL. Awali, wawili hao walikuwa wakisikika kila mmoja akidai hana tatizo na mwenzake huku chini ya kapeti zikiripotiwa habari za fukuto la bifu kali kati yao.

Jose Mourinho Kusimamishwa Kizimbani
Profesa: Trump anaweza kupokonywa urais kwa hili...