Majina ya Diamond na Ali Kiba katika Afrika Mashariki yanatafsiriwa kama majina ya mahasimu wakuu kwenye muziki Tanzania, lakini wawili hao wameendelea kuonesha kuwa hakuna uhasama kati yao.

Ali Kiba, hivi karibuni ameonesha ishara nyingine kuwa yeye na Diamond wana amani na kama ambavyo wawili hao wamekuwa wakieleza, ugomvi kati yao unachochewa na mashabiki kwenye mitandao ya kijamii lakini wao wako shwari.

Mkali huyo amepost picha kwenye Instagram akiwa na Diamond ndani ya vazi la team ya Bongo Fleva, picha iliyochukuliwa kitambo.

Ali kiba na Diamond

Zitto Awarushia Kombora Ukawa kuhusu Kilio cha Uteuzi Kamati za Bunge
'Zigo Remix' ya AY na Diamond yapigana vikumbo na nyimbo za Akon, Wiz Khalifa