Mkali wa Aje, Ali Kiba amelaani kitendo cha baadhi ya Watanzania kumshambulia msanii wa Nigeria, Wizkid kufuatia uamuzi wa MTV EMA kumpokonya tuzo msanii huyo na kumpa yeye.

Mwishoni mwa wiki hii, MTV EMA walikiri kufanya makosa na kumuomba Wizkid kuirejesha tuzo ya ‘Best African Act’ ambayo ilikabidhiwa rasmi kwa Ali Kiba.

Kupitia Instagram, Ali Kiba ameandika kwa lugha ya kiingereza ujumbe ambao tunautafsiri japo kwa tafsiri isiyo rasmi:

Sifurahishwi na kinachoendelea kwenye mitandao ya kijamii. Ninazo shukurani kubwa kwa @Wizkidayo kama msanii mwenzangu na kama shabiki. Nimekatishwa tamaa na kusikitishwa na mashambulizi ya matusi yanayoelekezwa kwake, na nataka nieleweke vizuri kuwa nalaani tabia hii na nina amini hakuna shabiki wangu wa kweli anayejihusisha na ujinga huu kwani wanajua siku zote nimekuwa na upendo kwa @wizkidayo.

Piga chini kelele kutoka kwa wenye chuki kaka, hongera kwa mwaka wako wa mafanikio. Mapenzi tele kutoka kwa mashabiki wa kweli na kutoka Tanzania. Pamoja #KingKiba.

Video: Sitta alifanya mabadiliko makubwa kwenye kanuni za Bunge - Msekwa
Chukua Hii: Wataalam watoa toleo la TV inayofukuza Mbu