Muda mfupi baada ya kuingia sokoni Album ya msanii wa mziki wa kizazi kipya nchini Ali Kiba  ” ONLY ONE KING” imefanikiwa kuweka rekodi ya kipekee kupitia mtandao wa ku-stream muziki online Apple Music.

Hii ni tangu iachiwe rasmi usiku wa kuamkia leo oktoba 6, 2021 ambapo chini ya masaa kumi na tano Album hiyo imefanikiwa kupenya na kuingia kwenye orodha ya Album zenye kufanya vizuri zaidi duniani kwenye mtandao huo mkubwa na maarufu Duniani.

Album hiyo imefanikiwa kukamata namba Moja ikifuatiwa na Album ya msanii Meek Mill ambaye ameshika namba mbili na Album yake mpya “EXPENSIVE PAIN”, tatu ikishikiliwa na Album ya Drake (CLB) “CETIFIED LOVER BOY”  Namba nne ni rapa Lil Nas X na Album yake iitwayo “MONTERO”

Kukaa kwenye nafasi hiyo ndani ya muda mfupi kwa msanii Ali kiba ndani ya muda mfupi inaonyesha taswira ya ukubwa na uzito wa Album hiyo “ONLY ONE KING” ambayo mpaka sasa wadau mbali mbali wa muziki wameendelea kumpongeza kwa kufurahishwa na uzuri wa kila wimbo unaopatikana katika Album hiyo.

Rais Samia Suluhu ampongeza Gurnah kutunukiwa Tuzo ya Nobel
Twiga Stars kuivaa Malawi