Mwimbaji Ali Kiba ameamua kutojikita katika kusaka tuzo za muziki zinazotolewa na makampuni pamoja na mashirikisho ya sanaa duniani kutokana na kuziona kama biashara zao.

Akiongea na BBC, Mwimbaji huyo ambaye wiki iliyopita alipata shavu la kuwa chini ya mwamvuli wa kampuni kubwa duniani ya kusimamia muziki, Sony Music aliwataka wasanii kujikita katika kufanya muziki mzuri na kutofikiria sana kuhusu tuzo kwa sababu “tuzo ni business”.

“Hata zamani hakukuwa na tuzo lakini wasanii waliokuwa wanafanya vizuri walionekana wanafanya vizuri tu,” alisema.

Katika hatua nyingine, King Kiba aliuelezea mkataba wake na Sony Music kuwa ni wa miaka mitano lakini utakuwa ukifanyiwa mapitio kila mwaka. Alisema kupitia dili hilo atatoa album itakayouzwa duniani kote ikiwa ni muziki wa kusikilizwa na kutazamwa (audio and video).

Ingawa Sony Music ilieleza kuwa Ali Kiba atafanya wimbo na msanii mkubwa wa Marekani hivi karibuni, msanii huyo hakuwa tayari kumtaja msanii huyo.

“Mipango ni mingi, lakini bado mapema sana siwezi kueleza. Hata kama ingekuwa tayari nisingesema kwa sababu mimi huwa napenda kuwapa surprises mashabiki wangu, there are many on process,” alisema Ali Kiba.

Maalim Seif Mikononi mwa Polisi
Ngamia mwenye hasira amuua na kumtafuna mmiliki wake, akerwa na tabia hii

Comments

comments