Hatimaye Ali Kiba amezungumzia sakata la mfanyabiashara wa mitumba kufungua shauri mahakamani akidai matunzo ya mtoto aliyempata na mwimbaji huyo. Mtoto huyo ana umri wa miaka mitano.

Akizungumza na Leo Tena ya Clouds FM leo akiwa pamoja na mkewe, King Kiba amekiri kuwa na mtoto na mfanyabiashara huyo wa mitumba aitwaye Hadija Hassan. Hata hivyo, amekanusha madai ya kumtelekeza mwanaye na kueleza kuwa amekuwa akitoa fedha kwa ajili ya matunzo ikiwa ni pamoja na ada ya shule.

“Mimi hilo nimeliona kwenye magazeti. Bado Mahakama haijaniletea wito wowote,” alisema Ali Kiba. “Lakini nimekuwa nikimhudumia siku zote mtoto, hata hivi karibuni nilimtoa kwenye shule ya chini kidogo nikamhamishia kwenye shule bora zaidi,” alisema Ali Kiba.

Mkali huyo wa Seduce Me alisema kuwa hafahamu kwanini mzazi mwenzake huyo ameamua kuchukua hatua hiyo, lakini aligusia kuwa Bi. Hadija alianza kuchukua hatua ambazo zilikuwa na muelekeo wa kuvuruga utaratibu wa matunzo ya mtoto hapo awali.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Bi. Halima alifungua kesi mahakamani akiiomba mahakama kumuamuru Ali Kiba kutoa kiasi cha sh 1.4 milioni, ikiwa ni pamoja na karo ya mtoto sh 950,000 kwa kila mhula.

Katika fedha hizo, Bi. Halima anamtaka Ali Kiba kuwa anatoa kiasi cha sh. 460,000 kila mwezi kwa ajili ya matunzo ya mtoto kwa maisha ya kawaida mbali na shule.

Ali Kiba ambaye amefunga ndoa hivi karibuni, amesema kuwa ana watoto watatu wa nje ya ndoa ambao mkewe anazo taarifa za uwepo wao.

“Mmoja ni mwanaume, yule aliyesoma dua kwenye harusi… wengine wawili ni watoto wa kike,” alisema Ali Kiba.

Mbunge wa viti maalum Chadema apata ajali
Mke wa Alikiba afunguka mazito, mengine ayaweka kando

Comments

comments