Msanii mahiri kutoka kwenye kiwanda cha muziki wa Bongo fleva Ali Kiba ametangazwa kuwa mmoja wa Mabalozi wa Kampeni maalumu ya usafi wa mazingira katika jiji la Dar es salam.

Katika hafla hiyo iliyoongozwa na mkuu wa mkoa wa Dar es salam Amos Makalla, msanii Ali Kiba alipata nafasi ya kuzungumza mambo kadhaa kuhusu nafasi aliyokabidhiwa na na mambo kadhaa anayoyaelewa kuhusu usafi na mazingira kwa ujumla wake.

“Shule zilitufundisha vitu vingi sana sisemi kwamba walifeli kwa upande mmoja lakini somo la uzalendo lingekuwepo mashuleni hizi Kampeni

zisingekuwepo leo, maana tungekuwa ndani yetu tunaona kabisa kwamba ni lazima ninapolala, ninapoishi, katika Mkoa wangu ningetamani uwe msafi kama Nchi nyingine za wenzetu huko nje”

“Usafi unaanza na wewe mwenyewe, nina imani kila Binadamu aliyekamilika kichwani kipaumbele cha kwanza ni usafi, usipofanya hivyo utaonekana wa tofauti na watakuuliza Watu”
Licha ya kuweka bayana matamanio yake juu ya namna wananchi wanavyopaswa kujali na kuyatunza mazingira yanayowazunguka Ali Kiba aliongeza kwa kumpongeza Mkuu wa Mkoa wa Dar es salam kwa kuamzisha kampeni hiyo kama sehemu ya kudhihirisha kuijali jamii na atakavyo itumia nafasi ya ubalozi kuhamasisha Usafi kuzingatiwa.

“Mimi ni Balozi lakini ningependa niwawakilishe Mabalozi wenzangu ambao ni Wananchi wanaoishi Dar es salaam ningependa tutambue kuwa usafi ni haki yako, usafi ni lazima, naomba mkuu wa Mkoa kama kungekuwa na uwezo wa kushtakiana kwa Mtu akiangusha uchafu apelekwe kwa sababu ni haki yako kutetea mazingira” aliongeza.

Ali Kiba ameteuliwa na  RC Makalla kuwa balozi katika kuchochea mafanikio ya kampeni hiyo akishirikiana ana Msanii Harmonize pamoja na Steve Nyerere.

Habari kubwa kwenye magazeti ya leo Novemba 23, 2021
Morrison aibwaga Young Africans CAS