Msanii mkongwe wa muziki wa bongo fleva, Ali Kiba leo akiwa na lebo yake  ya Kingi Music  ametambulisha rasmi wimbo wake wa ‘Mwambie sina’  wakati akifanya mahojiano na kipindi cha Leo tena cha clouds Fm.

Alikiba  ameelezea vitu vingi kuhusiana na  record lebo yake ya King Music  pamoja na ngoma yake ya hela ambayo iliachiwa  na baada ya muda kufutwa kwenye mtandao wa YouTube

Amesema lengo kubwa lilikuwa ni kutoa hela siku ya arobaini  ya dancer wake  aliyefariki na alifanya hivyo kumuenzi  kwani ndiye mtunzi wa staili zote  katika wimbo huo .

Aidha, amesema  hela ilitolewa kimakosa  na mtu ambae anahusika na YouTube ambapo aliitoa siku ya jumanne  siku ambayo huwa hatoi nyimbo ,hivyo wimbo huo haukuwa rasmi kama wangu  kwasababu nilikuwa na wimbo rasmi ambaao  ni “Mwambie Sina” amesema Alikiba.

“nilishawahi kuwa na lebo  lakini haikuwa rasmi ,wazo hili liliniijia wakati nipo G record niliona mimi nilivyosaidiwa  nikasema na mimi Allah akinijalia uwezo nitasidia vijana wengine, nimeamua kuwachukua vijana  hawa  kwanza kwasababu wanavipaji halisi ,wamefuzu vigezo  vyote vya muziki  nimekuwa nao kwa muda wa miaka miwili nikiwapika  sasaivi wapo tayari kuingia kwenye tasnia ya muziki rasmi” amemalizia kiba

Mbunge Neema azidi kumwaga misaada Njombe, agusa maisha ya wananchi
Shonza akerwa na watafuta kiki mtandaoni, Sister Fey atajwa

Comments

comments