Msajili wa Vyama vya siasa nchini, Jaji Francis Mutungi amewaandikia barua chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), akiwataka watoe maelezo kwa nini wasichukuliwe hatua kwa tuhuma za uvunjifu wa sheria na maadili ya vyama vya siasa.

Barua hiyo imebainisha kuwa Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe aliongea lugha za kuchochea vurugu katika mkutano wa hadhara wa kufunga kampeni za uchaguzi wa Ubungo na Kinondoni uliofanyika katika viwanja vya Mwananyamala kwa kopa jijini Dar es salaam.

Amesema mwisho wa kuwasilisha maombi hayo ni Tarehe 25, Februari 2018 na yafikishwe ofisini kwake.

Msajili amesema Mbowe alizungumza lugha za kuchochea vurugu amabazo zinakatazwa katika kifungu cha 9 (2) (f) cha Sheria ya vyama vya siasa Sura ya 258 (RE:2002) na kanuni ya (5)  (1) ya maadili ya Vyama vya siasa (GN.215-2007).

”Kila chama cha siasa kitakuwa na wajibu wa kutunza maadili chini ya kanuni hizi kwa kulaani, kuepuka na kuchukua hatua zitakazofaa, ili kuzuia kuepuka vitendo vy avurugu, uvunjifu wa amani au ukandamizaji wa ain ayeyote” amesisitiza Mutungi katika kanuni ya (5) Kifungu cha (1) cha sheria za vyama na kanuni za maadili ya Vyama vya siasa.

Ameongezea kuwa katika kanuni (6) (1) za maadili  ya vyama vya siasa katika kuhakikisha kanuni hizo zinatekelezwa, Msajili wa vyama atakuwa na wajibu wa kusimamia maadili ya vyama, kupokea malalamiko yaliyowasilishwa yanayohusu ukiukwaji wa maadili.

Hivyo amesema barua hiyo ni kwataka chadema kuwasilisha maelezo yao ni kwa nini walikiuka kanuni hizo na kwanini wasichukuliwe hatua madhubuti.

 

 

 

 

 

 

 

 

Mrema amjibu msajili wa vyama vya siasa, ''...hilo ni suala la polisi ''
T.I afunguka mpango wa kudhibiti umiliki silaha, 'watatuonea'