Vitimbi vya uchaguzi mkuu vinaendelea kuwa sehemu ya harakati za wagombea kuwaomba kura wananchi ambao kipindi hiki wanaonekana kama wafalme na malkia mbele yao.

Huko Muleba Kusini, mpiga debe wa mgombea ubunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya CCM, Profesa Anna Tibaijuka aliteleza ulimi wakati akimwagia sifa mgombea huyo akitoa mfano wa maisha yake alipokuwa naye ughaibuni.

“Nilishuhudia nikiwa Sweden alikuwa mwanamke pekee aliyepambana na miamba ya mataifa tofauti hadi akapata tuzo, kilichonishangaza Wazungu kumpigia magoti huyu mama. Sikuwahi kuona mwanamke wa Kiafrika ‘anafoka’ na kuwakimbiza lakini yeye ameweza,” alitiririka Katibu Mstaafu wa CCM Kagera, Faustin Kamaleki.

Ingawa Tibaijuka anachukuliwa kama Profesa aliyezaliwa kwenye kilindi cha kabila la wapenda kusifiwa na kujisifu, hiyo kwake haikuwa sifa bali ilikuwa mipondo ya mchana na hakuilazia damu alipopanda jukwaani.

“Huyu Kamaleki ameniponda kuwa ameniponda kuwa nilikuwa nawafokea wazungu, huwezi kuwafokea halafu wakakupa tuzo,” alisema Tibaijuka kwa mujibu wa Nipashe.

Aliendelea kufafanua kuwa wanachokifanya hivi sasa ni kuendelea kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM.

Tiffah Wa Diamond Aundiwa Kamati Maalum
Mgomo Wa Walimu Wafunga Shule Zote Kenya