Msanii wa nyimbo za Injili nchini, Goodluck Gozbert amesema kuwa kitendo cha kukutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli na viongozi wengine akiwepo Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete inamkumbusha watu ambao walikuwa wakimkatisha tamaa katika kazi yake hiyo.

Ameyasema hayo mara baada ya kupata nafasi ya kwenda Ikulu na kuimba mbele ya viongozi hao katika uzinduzi wa taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete Foundation.

“Nikukumbushe tu sikuzaliwa kwenye familia yenye kujulikana au kuwa na heshima kokote kule, na wala sikuwahi kushika hata nafasi ya tano darasani, nakumbuka kuchekwa, kukatishwa tamaa, kuandikiwa ubaya, kunenewa uongo na kutabiriwa kushindwa kila nilipofikiri ningeweza, nakumbuka mengi mengine ya juzi tu,”amesema Goodluck

Hata hivyo, Rais Dkt. Magufuli mara kadhaa alionyesha hisia zake juu ya nyimbo za msanii huyo na kusema kuwa anavutiwa sana hasa zaidi na wimbo wake ‘Hauwezi Kushindana’ ambao ameutoa mwezi wa tatu mwaka huu.

Young Africans kuifuata Wolaita Dicha kesho jumapili
DC Kasesela awafunda wasanii wa filamu nchini