Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amekubali uamuzi wa Rais Magufuli kumuondoa katika nafasi hiyo akisema kuwa Rais ndiye aliyemteua na sasa ameona ampumzishe.

Amesema, “Kwangu mimi hili ni jambo la faraja. Ninyi Waandishi wa Habari na Watanzania mmemsikia Rais hatua alizozichukua. Ni hatua nzuri zinalenga kujenga vizuri safu ya Serikali ya Awamu ya Tano.”

Aidha, ameongeza “Mawaziri waliopo, wanaoendelea waendelee kuchapa kazi. Likiundwa Baraza la Mawaziri na wachache kutoka CCM sisi wengine tuliopo benchi tunaendelea kuchapa jaramba unaweza kuingia muda wowote.”

Video: Rais Magufuli "Lugola nakupenda lakini kwa hili hapana"
Kliniki tembezi yanufaisha watanzania 200 Kiteto

Comments

comments