Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa pamoja na mkewe, Mama Regina Lowassa jana alimtembelea waziri mkuu mstaafu, Frederick Sumaye anaendelea kupata matibabu katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili akisumbuliwa tatizo la moyo.

Sumaye alieleza kuwa hali yake inaendelea kuimarika, maelezo ambayo pia yalithibitishwa na Kaimu Mkurugenzi wa JKCI, Profesa Mohamed Johabi.

Akizungumza baada ya kumjulia hali waziri mkuu mstaafu huyo, Lowassa alizungumzia kitendo cha viongozi wa ngazi za juu wa serikali akiwemo rais John Magufuli, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na rais Mstaafu, Jakaya Kikwete kumtembelea Sumaye kuwa ni kitendo cha uungwana, kuheshimiana na kutendeana mema.

Viongozi wengine waliofika kumjulia hali Sumaye kabla ya Lowassa na mkewe ni Waziri Mkuu Mstaafu, Dk. Salim Ahmed Salim na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Profesa Mwesiga Baregu.

 

 

Mahakama yatoa uamuzi kesi ya Uchaguzi wa Umeya, Ilala na Kinondoni
Nape awataka Chadema wamtimue Lowassa