Msanii wa kizazi kipya, Nick Mweusi maarufu kama Nikki wa  Pili, ametumia mitandao ya kijamii kutoa maoni  na mtazamo wake kuhusu tamko alilotoa Rais, John Pombe Magufuli, kuwa ndani ya utawala wake hakuna mwanafunzi atakayepata mimba na kuruhusiwa kurudi shule, hayo aliyazungumza katika ziara yake Mkoani Pwani.

Nikki wa pili ametweet ” Ukimpa mwanafunzi mimba baba jela miaka 30, mama anafukuzwa shule, huyu mtoto nae itakuwa ngumu pia kuepuka mimba ya utotoni”

”Mimba ndio njia ya kuja duniani na mwanamke ndio shujaa wetu daima nampa nyota begani,”

Lakini pia kupitia mtandao wake wa instagram Nikki wa Pili amedadafua swala hilo kiundani zaidi kwa kugusa sehemu ambazo zimesahaulika pindi uamuzi huo ulipokuwa unatolewa.

Nikki amesema, ”Huko uswahilini familia zimebaki na makovu ya kuwapoteza watoto wao walipokuwa wakijaribu kuwatowa ujauzito ili kuwaepusha na unyanyapaa wa kijamii kusemwa na kunyooshewa vidole,”

” Tafiti zinasema hata kwa watu wazima nao mimba nyingi ni zile zisizotarajiwa ndio maana mimba laki 5 hutolewa kila mwaka, kama wao linawashinda vipi kwa watoto.? ameuliza Nikki wa Pili.

”Namkubali sana Rais kwa mambo mengi mazuri na nia njema aliyonayo kwa watanzania, lakini hili la mimba sijui labda wazazi wenyewe watoe maoni yao,”.

”Mimi nadhani msichana mjamzito anahitaji kuelimishwa zaidi, kulindwa zaidi na kupewa msaada kisaikolojia maana kwenye jamii kuna unyanyapaa.”

Nikki ameuliza, Baba atafungwa jela, mama akifukuzwa shule mtoto atalelewa na nani? Hili swala linahitaji tafakari ya kina.

Fahamu ukweli juu ya omba omba tajiri duniani
Salah ajitia kitanzi Liverpool, aahidi makubwa EPL