Mwamuzi mstaafu Horacio Marcelo Elizondo kwa mara ya kwanza ameeleza kwa nini alimuonyesha kadi nyekundu Zinedine Zidane, wakati wa mchezo wa fainali ya michuano ya kombe la dunia mwaka 2006, kufuatia kitendo cha kumpiga kichwa Marco Materazzi.

Elizondo raia wa Argentina, amesema ilikua vigumu kuchukua maamuzi ya kumuonyesha kadi Zidane, kutokana na kutoliona tukio lililotokea dhidi ya Materazzi, hivyo ilimlazimu kuchukua muda na kutafuta ukweli wa mambo.

Mwamuzi huyo mstaafu mwenye umri wa miaka 55, amezungumzia tukio hilo katika mkutano maalum na waandishi wa habari uliofanyika nchini Argentina, ambapo amesema aliemuhakikishia nini kilitokea ni mwamuzi namba nne kutoka Hispania Luis Medina Cantalejo.

“Niliona Materazzi amelala chini, nilikua umbali wa mita 30 ama 40, nililazimika kusimamisha mchezo,” alisema Elizondo alipokua kaizungumza na waandishi wa habari.

“Kwanza nilijiuliza mimi binafsi, nini kimetokea?, lakini sikupata jibu sahihi.’

“Kwa haraka nilitumia mawasilino (intercom), nilimuuliza msaidizi wangu nini kimetokea?’

“Nilishangaa kupata jibu ambalo lilishabihiana na nilivyokua najihoji mimi mwenyewe binafsi, msaidizi wangu aliniambia hakuona chochote zaidi na yeye kujiuliza nini kimetokea.

“Bado niliendelea kujitafakari kwa kina, lakini nilijipa matumaini kuna tukio ambalo sio la kawaida limetokea.

“Ghafla nilisikia mwamuzi namnba nne Luis Medina Cantalejo akiniita ‘Horacio, Horacio, kuna tatizo, Zidane amempiga kichwa Materazzi, ndipo nilichukua jukumu la kutoa adhabu ya kadi nyekundu.

“Baadae nilipokua hotelini nilijiridhisha kwa kuangalia tukio lile kwa njia ya televisheni, na niliona ukweli wa mambo yote yaliyoendelea kabla na baada ya kumuadhibu Zidane!’

Katika mchezo huo Ufaransa walifungwa kwa penati, baada kwenda sare ya bao moja kwa moja dhidi ya Italia ndani ya dakika 120.

Hamisa atii amri awapigia magoti watanzania
Video: Steve Nyerere amjibu Muna Love