Msanii wa Bongo fleva Alikiba, amefanya mazungumzo na balozi wa Ufaransa Frederic Clavier leo Juni 17, 2019, ambapo wamekubaliana mambo mbalimbali ikiwemo kuendelea kubadilishana utamaduni.

Akiweka wazi mazungumzo yao, amefunguka haya, ”Tumezungumza mengi kuhusu namna gani tunaweza kujenga daraja la kubadilishana utamaduni baina ya Tanzania na Ufaransa”.

 

Alikiba ni miongoni mwa wasanii ambao huenda wakawa wanafahamu kidogo lugha ya Kifaransa ambapo amewahi kuimba baadhi ya mashairi yake kwa Kifaransa katika wimbo wake wa Aje.

Nguvu ya pesa ipo, lakini mkono wa Mungu hauepukiki- Makonda
Wema Sepetu aswekwa mahabusu