Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini anayefanya vizuri katika tasnia hiyo, Ali Kiba maarufu kama Mfamle Kiba amesema aliamua kutengeneza kinywaji cha ”Energy Drink” cha Mofaya yaani kinywaji cha kuleta nguvu kutokana na kwamba watanzania wengi wanafanya kazi na ili kuendana na kauli mbiu ya Rais John Pombe Magufuli ya hapa kazi tu hivyo kinywaji hiko kitawapa nguvu ya kufanya kazi kwa ubora zaidi.

”Mimi nimeona nilete kinywaji kuwapa nguvu kufanya kazi zaidi na kuamsha akili zetu ili kuleta ufanisi zaidi” amesema Alikiba.

Ameongezea kuwa wazo la Energy Drink limekuja kutokana na kazi yake ya muziki kwani mara zote kabla ya kupanda katika stage kufanya show hutumia kinywaji cha Energy Drink ili kumpa nguvu ya kufanya vizuri, na kutokea hapo aliona umuhimu wa kuwa na kinywaji chake mwenyewe ambacho kitatumiwa na watu wengi zaidi.

Alikiba amezungumza hayo mapema leo hii pindi alipohojiwa na moja ya chombo cha habari hapa jijini.

Aidha amekazia kwamba wapo watu wanaosema anaringa amefafanua na kudai kuwa yeye haringi ila anaishi maisha yake na si maisha ya kuigiza zaidi tu amesema anajipenda kama ambavyo kila mtu anapaswa kujipenda.

Hayo ni maneno ya watu tu lakini lazima mfahamu kwamba mimi siwezi kuishi maisha ya kuigiza. Mimi niko real, siringi lakini najipenda kama amabvyo kila mtu anapaswa kujipenda. Naheshimu mkubwa na mdogo , wakati mwingine watu wanatengeneza maneneo tu”. amesema Alikiba

 

Nchi hii inatia aibu kuagiza mafuta nje ya nchi- Zitto Kabwe
Eric Cantona kutua Old Trafford