Mkali wa wimbo Aje na mshindi wa  ‘MTV Europe Music Awards’, Alikiba amefungua mwaka kwa kutangaza ratiba ya kuizunguka sehemu ya dunia.

King Kiba alitumia nafasi ya kuwatakia   mashabiki wake heri ya mwaka mpya kwa kuwapa habari njema kuhusu ratiba ya kuizunguka dunia kwa lengo la kukutana na mashabiki wake walio nje ya mipaka ya Tanzanaia.

Muimbaji huyo ambaye mwaka 2016 ulikuwa mzuri kwa upande wake baada ya kuchukua tuzo 13 za kitaifa na kimataifa, Ameutaja mwezi Februari mwaka huu kuwa mwezi atakaoianza ziara hiyo nchini Afrika kusini na kuikamilisha mwezi aprili kwa kuizuru Marekani.

kiba

Akiwa Africa Kusini Kiba atatumbuiza katika maeneno tofauti ya majiji ya Johannesburg, Durban, Cape Town, Pretoria na Soweto

Huko Marekani ziara Kiba  atatumbuiza katika miji ya Las Vegas, Austin, Houston, Minneapolis na Minnesota katika.

 

 

 

Yanga yabonyezwa kifurushi cha 4G na Azam FC
Majaliwa awasweka ndani maafisa wanne Masasi