Ili biashara yako ikue na kufika mbali zaidi lazima uhitaji ushindani ambao ndani yake utakufanya usibweteke na ndio maana makampuni makubwa yanayotoa huduma moja hufanya kuboresha mifumo ya huduma zao ili kampuni isibwetweke na kuridhika.

utangulizi tuu katika kufikia lengo kuu kwa Wasanii Alikiba na Diamond ambao wao wenyewe wanakanusha haewana bifu kati yao ila mashabiki ndio wanaokuza chuki kwa kuwalinganisha na kuwashindanisha kuwa mmoja ni bora kuliko mwingine.

Alikiba na Diamond kwa mtazamo wa baadhi ya mashabiki wanaopenda maendeleo yao wanashauriwa kutengeneza pesa  kupitia udhaifu wa mashabiki zao kwa kuandaa  wimbo mkali kwa pamoja ili kudhihisha hawana tofauti na baadae wafanye show za pamoja ili kudhihirisha hawana tofauti.

Hilo linawezekana kwani hata mpenzi wa msanii Ali Kba ambaye ni mwanamitindo Jokate Mwegelo ameonesha kuwa hana tofauti na Ex wake Diamond kwa kusifia ubora wa uchezaji katika video yake mpya ya Kidogo ambapo ameonesha kutamani muungano wa wasanii hao.

Jokate

Mrembo Jokateanatamani amuone Diamond na Kiba kwenye ngoma moja.

“Naendelea kusubiri siku utakayo fanya kazi na team kiba tho- kiroho safi ?. Hongera kwa kazi nzuri dogo @diamondplatnumz.” aliandika Jokate.

Unaweza kujifunza kitu kuwa wasanii hawa wakawa hawana tofauti kwani Diamond Kampatia Kiba heshima ya kuweka picha yake katika ofisi ya WCB, Kiba aliwataka watanzania kumpigia kura diamond katika tuzo za BET zilizofanyika siku zilizopita.

Iliwahi kusemekana kuwa Vanessa Mdee ana ugomvi na Shilole lakini baadae walimaliza tofauti zao kwa kuandaa Shoo ya pamoja Billz Club wakatengeneza pesa, Wema Sepetu alishawahi kuwa na ugomvi na Jokate lakini walimaiza tofauti zao katika Show aliyokuwa ameeanda Jokate Arusha. Kiba na diamond pia wanauwezo wa kufanya hivi kwa kukusanya mashabiki zao kurudi na kuwa wamoja.

Zinedine Zidane Afunguka Kuhusu Paul Pogba
Per Mertesacker: Granit Xhaka Ni Chaguo Sahihi Kwa Arsenal