Baada ya kuanza vibaya Michuano ya Kombe la Dunia 2022, Kocha Mkuu wa Senegal Alious Cisse amesema anapaswa yeye kama Mkuu wa Benchi la Ufundi na sio wachezaji wake.

Senegal ipoteza mchezo wake wa kwanza wa Kundi A kwa kufungwa na Uholanzi Mabao 2-0 jana Jumatatu (Novemba 21), katika Uwanja wa Al Thumama, mjini Doha.

Cisse amesema Wachezaji wake hawapaswi kulaumuwa na yoyote aliyechukizwa na matokeo ya mchezo huo, badala yake lawama zote zielekezwe kwake kwa sababu alifanya maamuzi ya kila hatua walioipiga kwenye mchezo huo.

Amesema ikitokea Wachezaji wakaendelea kulaumiwa watakua wanakosewa sana, hivyo amesisitiza yeye kama Kocha Mkuu anapaswa lawama hizo na ikiwezekana akiulizwa ataweza kuzitolea ufafanuzi.

“Ninaweza kuwa mimi ndio mkosaji mkubwa kwa sababu mimi ndiye Kocha Mkuu. Ukishindwa lazima useme shida ni kocha. Mpira ni ufanisi, usipofunga huwezi kushinda.” amesema Cisse

Senegal iliweza kulinda isifungwe hadi dakika ya 83′ ya mchezo, lakini kwa bahati mbaya waliruhusu kupoteza kwa mabao ya Cody Mathès Gakpo na Davy Klaassen yaliyofungwa dakika ya 84 na 90+ 9.

Ushindi wa Uholanzi unalifanya Kundi A kuwa na ushindani mkubwa kwani hadi sasa taifa hilo la Ulaya limefungana kwa alama na mabao ya kufunga na Ecuador, huku wenyeji QATAR na Senegal wakiburuza mkia wa Kundi hilo.

Jezi ya Ubelgiji yapigwa marufuku QATAR
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Novemba 22, 2022