Mwandishi wa kitabu kilichokuwa kikituhumu uwepo wa wizi wa kura katika chaguzi zote za Kenya tangu ukomo wa utawala wa Rais wa zamani wa nchi hiyo, Daniel Arap Moi anadaiwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha.

Kwa mujibu wa Daily Nation, kijana huyo ambaye anafahamika kwa jina la Newton Babior aliyeandika kitabu hicho alichokiita ‘Raila Odinga, The People’s President’ alipotea katika siku aliyokuwa amepanga kukizindua kitabu hicho kwenye ukumbi wa KICC, Juni 27.

Mtu wake wa karibu aliiambia Daily Nation kuwa simu za Babior hazipatikani tangu siku hiyo, na kwamba tukio la kupotea kwake liliripotiwa katika kituo cha polisi cha Ruaraka.

“Uzinduzi ulipangwa kufanyika siku hiyo lakini Bobior alipotea wakati wa maandalizi na hatumpati tangu siku hiyo,” alisema Vincent Adede, meneja wa Booksaves.

Uzinduzi huo unadaiwa kuwa ungehudhuriwa na mgombea urais kwa tiketi ya NASA, Raila Odinga, Profesa Lumumba wa chuo kikuu cha cha sheria cha Kenya na mchambuzi wa masuala ya kisiasa wa Chuo Kikuu cha Nairobi, Herman Manyora.

Majira ya saa nne asubuhi ya siku aliyopotea, Babior aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook ujumbe wa kuwahamasisha wakenya huhudhuria uzinduzi wa kitabu chake.

Mshambuliaji Yanga atakiwa Tottenham Hotspur ya Uingereza
Raila Odinga aishukia tena Tume ya uchaguzi Kenya, adai kubaini mbinu chafu