Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbroard Mutafungwa amesema kijana Kennedy Nyangige (20) mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Afya Bugando (Cuhas) aliyetoa taarifa za uongo kwa familia yake kwamba ametekwa na watu wasiofahamika na yupo sehemu isiyojulikana anashikiliwa na Polisi mkoni humo.

Kamanda Mutafungwa amesema kijana huyo alitoa taarifa kutumia simu yake kuwa watekaji walitaka watumiwe mil 3.5 ili wamuachie vinginevyo angeuawa.

Mkoa wa Mwanza

Aidha amesema kuwa baada ya taarifa hiyo kuripotiwa polisi, walianza uchunguzi wa kina na kumkuta kijana huyo katika nyumba ya wageni iitwayo Fm Katapila iliyopo Kata ya Igogo, wilayani Nyamagana, akiwa amejifungia ndani chumba namba 103, huku akiendelea kunywa pombe.

Bashe azindua kongamano la usalama wa chakula
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Mei 14, 2023