Katika kisa cha kusikitisha kilichotokea huko Marekani, mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la David Riston aliyekuwa amewafuga zaidi ya nyoka 100 amefariki nyumbani kwake katika jimbo la Maryland nchini Marekani.

Maafisa wa polisi katika jimbo hilo wameviambia vyombo vya habari kuwa kifo cha David Riston, mwenye umri wa miaka 49, kimetokana na kung’atwa na nyoka kwa bahati mbaya.

Taarifa ya maafisa wa upelelezi wa Maryland inasema mwili wa marehemu ulipatikana ukiwa pamoja na nyoka 124 nyumbani kwake.

“Hakuna aliyeonekana kufahamu kuwa alikuwa akihifadhi nyoka ndani ya nyumba,” msemaji wa Kaunti ya Charles Jennifer Harris alisema wakati huo.

Kwa mujibu wa NBC News, nyoka hao wamo wenye sumu kali(cobra), chatu wa Burma mwenye urefu wa futi 14 na black mamba ambao walisababisha zoezi la kuuokoa mwili wake mmiliki wao kuchukua saa kadhaa na Mmoja wa nyoka hao anashukiwa kumuua Riston

“Ni Wakati wa Kupona Vidonda” Msemaji wa Idara ya Afya ya jimbo hilo, alisema katika barua pepe kwamba uchunguzi wa maiti ulionyesha kuwa kifo cha Riston kilikuwa cha bahati mbaya kilichosababishwa na sumu ya nyoka.

Dkt.Kijaji: Anayekwamisha utalii na uwekezaji, atakuwa mfano
Chinga aliyenyang'anywa ndizi asherehekea Pasaka ya viwango vya juu