Kweli dunia ina mambo; maajabu hayatakwisha hadi ajabu la mwisho la kiama. Hivyo ndivyo unavyoweza kusema baada ya kusoma habari hii ya mwanaume mmoja aliyefunga ndoa na kompyuta mpakato ‘laptop’ na kisha kukimbilia mahakamani.

Kwa mujibu wa Washington Post, mwanaume huyo aliyetajwa kwa jina la Chris Sevier alifunga ndoa na laptop yake na kufanya sherehe kubwa nchini Marekani katika eneo la New Mexico.

Sevier ameamua kufungua kesi mahakamani dhidi ya Serikali akitaka ndoa yake iweze kutambulika kisheria kwa madai kuwa kama nchi hiyo inakubali ndoa za jinsia moja kwanini isikubali ndoa ya mtu na mashine yake.

Katika maombi yake ya kufungua kesi, Sevier pia ameijumuisha kampuni maarufu ya kuandaa keki za harusi ya Colorado kwa kukataa kumuandalia keki maalum ya ndoa yake na laptop hiyo.

Jaji wa Mahakama ya jimbo la Utah, Magharibi mwa Marekani amekubali ombi hilo la mashtaka kuendelea na mchakato wa kimahakama.

Haijafahamika mara moja sababu za Sevier kuchukua uamuzi wa kufunga ndoa na kifaa hicho.

NB: Picha sio ya mhusika

August Alsina amaliza bifu na mama yake mzazi jukwaani
Barcelona kuishtaki PSG, wahofia walikotoa fedha kumnasa Neymar