Mtuhumiwa namba moja ambaye amehusishwa na kifo cha msanii wa muziki nchini Uganda, Mowzey Radio amekamatwa na Jeshi la Polisi nchini humo.

Wamala Godfrey mwenye umri wa miaka 28 ambaye amekuwa akisakwa na polisi kama mtuhumiwa mkuu mara baada ya mmiliki wa bar, Egesa George na Meneja wake kushikiliwa na polisi baada ya kifo cha Radio kutokea.

Wamala amekamatwa katika eneo la Kyengera nyumbani kwa rafiki yake alipokuwa amejifiicha kwa siku kadhaa, Na sasa Wamala amehamishwa mjini Entebe.

Mwimbaji Mowzey Radio alifariki dunia Februari Mosi mwaka huu kutokana na majeraha ambayo aliyapata kichwani kufuatia ugomvi katika bar hiyo.

Inasemekana kuwa ugomvi huo umetokea mara baada ya msanii huyo kuletewa kinywaji kilichofunguliwa, katika harakati za kukataa kinywaji hicho, marehemu Radio alichukua uamuzi wa kukimwaga ndipo ugomvi mkubwa ulipotokea na kusababisha mlinzi wa bar hiyoA kumtembezea kipigo cha mbwa mwitu marehemu Radio na kumsababishia kuvunjika shingo na fuvu lakichwa na umauti kumkuta.

Kamanda wa Polisi Kampala, CP. Frank Mwesigwa amethibitisha kushikiliwa kwa Wamala Godfrey na kueleza kuwa kwa sasa wanaandaa majalada ili kuweza kumfikisha mahakamani.

Mtoto amuua mdogo wake wa miaka 2 kwa risasi, ajiua
Sheikh Mkuu ampa onyo kali Mange Kimambi