Sauti ya Wakenye kupitia mitandao ya kijamii imemnusuru mwanaume mmoja aliyehukumiwa mahakamani kwa kosa la kujaribu kumtorosha mwanaye aliyetibiwa katika Hospitali ya Taifa ya Kenyatta, akikwepa kulipa Ksh. 56,937 (sawa na Sh 1,325,060 za Tanzania).

Boniface Murage anadaiwa kufanya kosa hilo Februari 16 mwaka huu, baada ya mwanaye kupatiwa matibabu na kuwasilishiwa bili hiyo.

Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Milimani, ilimkuta na hatia lakini kutokana na msaada wa kisheria aliopewa na Mbunge wa Embakasi Mashariki, Babu Awino, aliachiwa na kuwekwa chini ya ungalizi wa serikali kwa kipindi cha miezi mitatu.

Kelele za Wakenya zimewaamsha viongozi mbalimbali na kuzua mijadala mingi, ambapo jana, Gavana wa Nairobi, Mike Sonko alijitokeza kumsaidia Murage kwa kumpa kazi/ajira pamoja na kufanya manunuzi ya mahitaji ya mtoto.

Kwa mujibu wa Citizen, timu ya Gavana Sonko ilimpeleka ‘shopping’ mke wa Murage kwa ajili ya kununua vifaa vyote muhimu vya mtoto pamoja na familia kwa ujumla.

Kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, Sonko alisema kuwa atamsaidia Murage kupata kazi katika idara ya mazingira nchini humo. Sehemu ya gharama anazodaiwa hospitalini zililipwa kwa kuchangiwa na wasamaria wema. Sonko ameahidi kushiriki kumalizia malipo ya gharama hizo.

Maalim Seif ajipanga kuunda ‘CUF Mpya’
Meneja afia kwenye kiti akizungumza na waandishi wa habari

Comments

comments