Mwanasheria wa haki za binadamu nchini China, Pu Zhiqiang anakabiliwa na mashtaka baada ya kukosoa mwenendo wa chama tawala nchini humo.

Pu Zhiqiang
Kwa mujibu wa duru kutoka nchini humo, mwanasheria huyo wa haki za binadamu alikikosoa chama cha kikomunist kupitia mitandao ya kijamii.
Chanzo cha kuaminika kimeiambia BBC kuwa hakuna dalili za kumuachia huru mwanasheria huyo na kwana anaweza kufungwa hadi miaka nane gerezani kwa mujibu wa sheria za nchi hiyo.