Baada ya uvumi wa kifo cha Mwanamuziki Shatta Wale kutoka nchini Ghana na Jeshi la polisi kutangaza kuingia katika kufanya uchunguzi wa kina juu ya taarifa hizo, hatimaye Jeshi la Polisi nchini humo limefanikiwa kumpata Shatta Wale na kumtia mbaroni kwa madai ya kusambaza taarifa zisizo za ukweli na kuzua taharuki katika jamii.

Siku ya Jana octoba 19, 2021 zilienea taarifa zikidai mwanamuziki huyo ameshambuliwa kwa risasi na pengine huenda akawa amefariki dunia muda mchache baadae huko East Legon Ghana.

Baada ya taarifa za kifo cha msanii huyo kuzua taharuki kwa wananchi wa Ghana na mataifa kadhaa ya Afrika hasa kupitia mitandao ya kijamii, Jeshi la Polisi nchini humo lilijitokeza na kutangaza hadharani kuanza uchunguzi ili kufahamu alipo msanii huyo ili kujua ikiwa ni kweli amekufa au La.

Mapema asubuhi ya leo octoba 20,2021 imeelezwa kupitia ukurasa maalumu wa mtandao Facebook jeshi hilo, kuwa Shatta Wale mwenyewe alifika kituoni kujisalimisha.

Polisi nchini Ghana wamethibitisha kumtia nguvuni msanii huyo ili kuanza kufuata taratibu za kisheria kulingana na kesi inayomkabili.

Wachezaji wamfariji Paul Godfrey Boxer
Rais Ndayishimiye kuwasili nchini kesho